Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe, ameomba mwongozo kuahirishwa kwa Bunge ili kutoa nafasi ya Wabunge wote kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea.

Akiomba Mwongozo kwa Naibu Spika, Hussein Bashe amedai kuwa amefahamishwa na baadhi ya Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kuna kikundi ambacho kinahusika na utekaji wa watu. Amedai kuwa kuna Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa na kuondolewa uhai. Mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie

“Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie. Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana”.

 

Kwa hapa tulipofika, ni wazi kuwa JPM ajitafakari na baadhi ya watu wanaomzunguka.Kuna hali ya tahayari katika Taifa.

SOMA NA HII:  Hali ni mbaya sana kwa tovuti za Pirates na wazee wa Torrent

Jana nimeongea na Askofu mmoja wa Kikatoliki, nimeona dalili ya uhusiano wa JPM na Kanisa kudorora kwa namna anavyoendesha mambo ya Nchi.

Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana’

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako