Sambaza:

Kwa nini unafanya unachokifanya ? Kweli, Ningependa kujua. Ni kitu gani kilichokusukuma wewe kutumia muda wako na nguvu katika shughuli hii? Je, ni hamu ya kupata utajiri ? ngono ? Kuonyesha mtu kuwa unaweza? Au kuna nguvu ndani yako inayofanya ufanya hivyo, ni rahisi kama hivyo ? Kitu gani kinafanya ufanye unachokifanya ?

Swali jingine, kwa motisha iliyomo ndani ya akili yako, unategemea kupeleka wapi kitu unachokifanya, na upo karibu kiasi gani kufika huko ?

Imewahi kusemwa kila binadamu anaona sehemu nyingine ni bora zaidi kuliko alipo yeye, na sipo hapa kusema huo ni uongo. Naishi Tanga na kama ninavyoujua mji wangu, kama ninavyoupenda mji wangu na wakati mwingine nchi yangu kwa kile inachotoa, mara nyingine napatwa na kuchanganyikiwa. Nawajua watu wengi wenye vipaji ambao wanapuuzwa, na umma na mara nyingi ni zaidi kuliko ilivyo kwa wao wenyewe. Watu ambao wanashindwa kuwa na mawazo ya kujitegemea kitabia siku zote hawafanikiwi. Kiasi kikubwa kati yao ni wasanii maarufu na watu wakubwa kwenye haiba hii ambao kila siku wanalalamika kutopata fursa na kutengwa, na ni kweli. Zaidi ya watu wanavyokuwa na wasiwasi kuwekeza fedha zao katika miradi yenu.

Kwa nini?

Mimi sijui na sitajifanya najua. Labda wanafikiri kuwekeza katika sanaa nchini Tanzania ni uwekezaji mbaya, yani kama vile ubunifu, umekwenda kila mahali kuacha vipande vyake na miujiza iliyosambaa juu ya meza. Labda ni utani wa ndani na watu wote katika Ofisi kubwa wanajiweka mbali na jitihada za Vijana, wakitusihi “Tuendelea kujaribu” huku wakiwa hawana msaada wowote. Labda ni mtihani.

Labda ni ujinga tu.

Vyovyote vile inaweza kuwa, hivyo ndivyo ilivyo ; Na hapo ndipo unapoweza kutofauti wakweli na waongo , kwa ukosefu wa njia bora ya kufanya kazi, kwa sasa.

SOMA NA HII:  Kuweka Mkeka "Kubeti" Njia ya Kutengeneza Pesa yenye Ugonjwa

Sikia hii; Unaweza kutengeneza ukurasa wako wa Facebook. Ukapakia picha yako na ya “Squad” yako , ukiongea jinsi ulivyo kwenye msako na “Upo hapa kujaribu kupata njia yako” huku ukiweka “hashtag” ya ukurasa wako wa Reverbnation wenye wafuasi wachache na mpenzi wako wa Facebook kama hicho ndicho unachotaka kufanya. Ni sawa kwa sababu hapo ndipo utakapo ishia; Unapata kile unachokitoa, na mimi naweza kuishia hapa lakini nasonga mbele na kusema: Kuwa mwaminifu kwa kile unachokifanya.

Hii inafahamika?

Ni ujinga, sio ? Mimi kuwaomba wasanii kuwa waaminifu katika nyakati na kizazi cha sasa , hasa wale ambao kimuziki wanaimani, lakini wapo kwenye jehanamu ya muziki. Kutokuwa na nia kunajitokeza mala nyingi na ukiwa mtu ambaye kila siku unaongelea jinsi unavyosonga mbele bila ya kuwa na chochote cha kuonyesha, sio tu inafanya uonekane mwongo, unaonekana mpumbavu. Hii lazima itabadili mtazamo wako kama umesoma hadi kufika hapa, najua wengi wenu hamjali kuonekana sio wakweli, unasema unatengeneza picha, ila kuonekana kama mjinga kutafanya ujisikie kama umeachwa njiapanda.

Watu wanafikiri kuchagua kazi ndani ya sanaa ni njia rahisi ya kutoka, yani kama kuma formula ya kushinda na inabidi nikubali wajinga wengi wenye vipaji feki “wamefanikiwa” ila sio hapa, hapa sio rahisi hivyo, na uko wapi tena? HAPA. Miujiza yako haiwezi kufanya kazi kwa watu ambao tayari hawataki kukusaidia. Bila ya kuwa na kipaji hakuta fanya upate ushindi mbele za watu kwa kuwadanganya , wanaona kile unachokifanya na utakuwa sehemu yao ya utani, na sasa, watu watajua haupo kabisa kwenye maisha hayo. Halafu nini kinafata?

SOMA NA HII:  Kukua Kwa Teknolojia na Kazi 7 Zinazoelekea Kutoweka

Watu ambao mioyo yao ipo ndani ya sanaa ndio wanajua umuhimu wa kupenda kile unachokifanya kabla ya vitu vingine vyote. Hilo ni jambo la kwanza, kabla ya mwonekana wako, kabla ya shabiki wako wa kwanza, Kabla hata hujafikiria kuwa mtu maarufu, kuna mapenzi. Umejitoa kwajili ya hilo; Inatumia muda wako, upendo wako, mawazo yako,inakuwa wewe, hata kama kamwe hutapata tuzo angalau moja kwa ajili ya hilo, hujapata utambulisho wowote kwenye “mainstream”, bado unafanya. Unafanya kwa sababu inakulazimu kufanya, huwezi kuishi bila sanaa.

Hakuna mtu anayetakiwa kukulazimisha kufanya kazi kwa sababu unafanya , hata kwenye siku ambazo ni mbaya kwako, unafanya.

Ila wengi wenu hamjui hilo, na nina mashaka kama mtakuja kujua.

Vitu vinavyozingatiwa nashindwa kuelewa wasanii wengi wanaongea kwa sauti ya kujiamini kuhusu jinsi wanavyokaribia kupiga hatua kubwa , na hakuna hata mmoja kati yenu mwenye kitu cha ziada cha kuonyesha zaidi ya ukurasa wa Facebook na downloads 300 za muziki wako. Ni kweli unafanya kazi na kupambana? Unawekeza muda wako? Unakutana na kukatishwa tamaa ama anguko la kiakili na bado unajiinua mwenyewe na kuendelea kufanya kazi?

Je, unajua kuwa machozi, jasho na damu sio mfano tu wa kwenye maongezi yetu ?

Kwenye tuzo nyingi nje ya nchi yetu hakuna wasanii wengi kutoka nchini, na siwezi sema nashangazwa na jambo hilo, ila inanikatisha tamaa. Kikweli nchi nyingi za Afrika hazina wawakilishi imara, turudi nyumbani Kuna wasanii wachache hapa kwetu ambao nahisi naweza kufanya vyema kwenye orodha hizi, na sijui nini kinawakwamisha. Sijui kama wanafanya kazi kwa nguvu zote, ama wanatumia nguvu zote katika sehemu sahihi, au hatuwapi msaada wa kutosha , sijui ila najua hili : Watanzania wanapenda kuwa nyuma ya mafanikio yako baada ya kufanikiwa.

SOMA NA HII:  Mfahamu Mwanzilishi Wa Kampuni ya Simu za Tecno - Tecno Mobile

Nimejadili jambo hili na baadhi ya wasanii niliowataja hapo mwanzo kwenye makala hii pia na watu wengine ambao hawajihusishi na jambo lolote kwenye sanaa na tumekubaliana juu ya jambo hili: Katika nchi hii inaonekana, Watanzania hawatoi msaada mpaka utakapopata utambuzi mahali pengine. Unaweza kupata mashabiki wachache hapa lakini angalia watakavyoongezeka kwa kasi zaidi watu kutoka nchi nyingine watakapo anza kukupa heshima unayostahili, heshima uliyoifanyia kazi kwa bidii. Ni kama wazazi ambao siku zote wanakuambia wewe hauna maana yoyote hadi utakapo kukutana na mtu ambaye atafanya ndoto zako kuwa kweli na wazazi wataanza kusema “siku zote walijua utafika mbali”.” Na hivyo ndivyo ilivyo”, watu wengi hawawezi kusema ukweli kuhusu hilo lakini ndivyo ilivyo na jambo hili lipo kila mahari.

Hata hivyo kukosekana kwa msaada, mimi nadhani hakuwezi kukurudisha nyuma, hakuwezi kudhoofisha mipango yako, inaweza tu kuichelewesha. Hata hivyo hiyo sio sababu ya kufanya ushindwe kufanikiwa, kama wewe ni msanii wa kweli unatakiwa kuwa na uwezo wa kuishi kwa kukabiliana na hali ilivyo. Sisi ni mende wa jamii yetu. kwa hiyo ni nini udhuru yako ? sababu ya kwa nini haupo kama ulivyokuwa unatuambia kwa miaka mingi? Unafanya nini?

Kwa nini bado wewe ni msanii asiye fahamika mwenye mdomo mkubwa huku hakuna kitu chochote kwenye wasifu wako?

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako