Barakah The Prince : Wewe ni nani sasa mpaka unipangie maisha?’


Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio msanii wa muziki Barakah The Prince amewaambia mashabiki wasimpangie maisha binafsi.

Muimbaji huyo ametoa kauli hiyo baada ya kushambuliwa na baadhi ya mashabiki ambao walimuita msaliti kwa kuonekana amepiga picha na meneja wa “Diamond” .

“Wewe kama ni shabiki wangu wa muziki haimaanishi pia ni shabiki wa maisha yangu binafsi, maisha yangu binafsi mniachie. Shabiki wewe ni nani sasa mpaka unipangie maisha? kama mtu niliyepiga naye picha ni binadamu siyo shetani lakini cha ajabu mashabiki ndiyo wanaonitukana na kuongea hivi na vile wakati uongozi wangu haujasema kama nakosea,”

Katika mahojiano hayo, Baraka ameweka wazi kuwa tangu kusajiliwa katika lebo ya Rock Star chini ya Bi. Seven Mosha kumemuongezea nafasi na wigo mpana wa kujulikana ndani na nje ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani kubwa katika maisha yake.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA