Hivi sasa kuna programu nyingi zinazazopatikana kwenye intaneti ambazo zinaweza kubadilisha mwonekano wa kompyuta yako kuwa unaovutia na pia kufanya iwe rahisi kuitumia.

Tunapenda Kompyuta zetu ziwe safi na zenye mafaili yaliyo pangiliwa vizuri  ili iwe rahisi kutumia vitu mbalimbali ndani ya Komyuta yako ama kutafuta “faili / folda kwenye Kompyuta kwa urahisi zaidi.

Sawa, hapa nakusogezea programu ambayo itakuwezesha kubadilisha rangi za folda zako kwenye kompyuta kuwa katika mfumo wa rangi unazozipenda hivyo kuwa rahisi kuzitumia.

Unawezaje Kubadilisha rangi ya “folders” kuwa na rangi tofauti ?


Ni rahisi, fata hatua hizi kubadilisha rangi ya folda zako kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu:

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuflash Simu za Tecno kwa Urahisi

Hatua ya 1 :

Kwanza pakua/shusha na kisha “install” programu ya  FolderColorizer. Ni salama na haiwezi kuleta madhara ya kiusalama kwenye Komyuta yako. Unaweza kupakua kwa kubonyeza : DOWNLOAD FOLDERCOLORIZER

Hatua ya 2 :

Baada ya kuinstall programu hii, bonyeza  “right click” kwenye folda lolote lile unalotaka kulibadilisha rangi. Hapa uki-right click kwenye folda, utakutana na chaguo jipya kwenye “context menu” nayo ni Colorize !. Nenda kwenye chaguo hilo na menyu nyingine itaonekana. Hapo unaweza kuchagua rangi yoyote unayotaka kwajili ya folda hilo.

Ingawa programu hii ni bure kabisa kuitumia ila unavyoitumia kwa mara ya kwanza , itatakiwa utumie barua pepe yako kufanya activation ya progamu hii. Ila hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwa sababu sio lazima ufanye activation kwa kuingia kwenye barua pepe yako. Kwa sababu usajili wa programu hii itakuwa umekamilika utakapo ingiza barua pepe yako.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kubadili mpangilio wa keyboard ya kompyuta kuwa Dvorak keyboard

Kwa ufafanuzi zaidi nimekuwekea”screenshot” ya hatua nilizozielezea hapo juu jinsi ya kubadilisha rangi za folda :

 

Kwa njia hii itakuwa rahisi kupangilia folda zako kwenye drive iwe ni C: , D: ama drive nyingine .

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako