Programu

Badilisha Partition kutoka NTFS hadi FAT32 bila Uharibifu wa Data

Ikiwa unahitaji kufikia faili fulani kutoka kwenye DOS mode au Windows 9X, unatakiwa kutumia mfumo wa faili wa FAT32. FAT32 ni mfumo wa faili wa zamani ikilinganishwa na NTFS, lakini ni rahisi na unatumika kwenye idadi kubwa ya mifumo ya uendeshaji (operating systems), na pia inasaidiwa na huduma mbalimbali za mfumo (system utilities). FAT32 inaweza kufanya kazi vizuri kwenye DOS v7 na mifumo ya juu ya Windows 98, ME, 2000, nk.

NTFS to FAT32 Converter ambayo imeundwa na AOMEI Tech Co, Ltd ni “file system conversion tool” ya bure (pia ipo ya kulipia). Inaweza kubadilisha kwa urahisi NTFS kuwa FAT32 bila kupoteza data, na inasaidia hadi ukubwa wa kuhifadhi wa 2TB. Zaidi ya hayo, pia inaweza kubadilisha FAT au FAT 32 kuwa NTFS bila kuingilia data zako.

Kubadilisha NTFS Kuwa FAT32

Hatua ya 1. Fungua AOMEI Partition Assistant, tafuta na bonyeza NTFS to FAT32 Converter upande wa kushoto wa dirisha kuu.

Hatua ya 2.Katika ukurasa utakao funguka, chagua NTFS to FAT32 na kisha bofya Next.

Hatua ya 3. Chagua partition ambayo unataka kuibadilisha. G partition kwa mfano.

Hatua ya 4. Utapata maelezo ya kukushauri uangalie partition yenye chkdsk.exe kabla ya kubonyeza kuendelea. Bonyeza Proceed kila kitu kikiwa tayari. Baada ya hapo, mfumo utakuongoza kukamilisha operesheni hii.

SOMA NA HII:  Usiyoyajua kuhusu program mpya ya Apple – iOS 11

Hatua ya 5. Na kisha bonyeza Finish.

Kumbuka:

AOMEI Partition Assistant inaweza kubadili kwa urahisi partition yako kuwa kwenye mfumo mpya wa faili wa FAT32 hata kama ilitumia NTFS kabla. Aina hii ya kufanya mabadiliko itaweka salama maudhui yaliyomo ndani ya partition husika.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Toa Maoni Hapa:

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako