Baba mzazi wa Belle 9 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, meneja wake, Jahz Zamba, amethibitisha taarifa hizo na. Chanzo cha kifo chake ni kugongwa na boda boda iliyokuwa kwenye mwendo mkali huko mjini Morogoro alikokuwa anaishi.

Alivunja mguu mmoja pale pale na kujeruhiwa vibaya kabla ya kupelekwa hospitali. Dereva wa boda boda naye ameumia vibaya ikiwemo kuvunjika taya na kujeruhiwa kichwa. Jahz amesema baada ya Mzee Damian kupelekwa hospitali na kuwekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahtuti, kuna dawa zilikuwa zikihitajika lakini zilikosekana kwenye hospitali hiyo. Amesema kaka yake Belle anayeishi Morogoro aliingia mtaani kuzisaka na aliporudi mida ya saa sita usiku alikuta Mzee ameshafariki.

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya Tecno S1 na Bei yake Nchini Tanzania

Mediahuru inampa pole Belle kwa msiba huo na Mungu ailaze roho ya Mzee Damian mahala pema peponi.

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako