Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu Essien amepata timu

Comment

Mchezaji wa zamani vilabu vya Chelsea ya England na Real Madrid ya Hispania Michael Essien leo March 14 2017 ametangaza kujiunga rasmi na timu ya Persib Bandung ya Indonesia baada ya kuwa nje ya uwanja bila timu kwa miezi sita.

Michael Essien mwenye umri wa miaka 34, baada ya kuachana na klabu ya Panathinaikos ya Ugiriki mwaka 2016 na muda wote huo amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha akiba cha Chelsea kabla ya kujiunga na Persib Bandung.

Michael Essien mwenye umri wa miaka 34 alikataa kujiunga na Melbourne ya Australia mwezi December mwaka jana, Essien amewahi kuichezea Chelsea ya England kwa misimu nane.

Up Next

Related Posts

Discussion about this post

error: Content is protected !!