Nyingine

Baada ya Kufanya Vizuri FIFA yatangaza neema kwa Tanzania

Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kushuka mfululizo katika viwango vya soka dunia vinavyolewa kila baada ya mwisho wa mwezi na FIFA, leo April 6, Tanzania imepanda juu kwa nafasi 22.

Tanzania kwa sasa imefanikiwa kusogea hadi nafasi ya 135 kutoka nafasi ya 157 yaani imepanda kwa nafasi 22.

Mwezi March Tanzania imecheza mechi mbili ambazo ni dhidi ya Burundi ikashinda kwa goli 2-1 na dhidi ya Botswana iliyoshinda kwa goli 2-0.

Tanzania wakati inakutana na Burundi walikuwa katika nafasi ya 139 na imeshuka hadi nafasi ya 141 wakati Botswana ilikuwa 116 na imeshuka hadi 120.

SOMA NA HII:  Swali la Siku: - Kati ya Vitu Hivi 3, Ni Kitu Gani Ni Ngumu Kwako Kuishi Bila Kukifanya?

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako