Home Nyingine Asilimia 94 ya bomba la gesi haina matumizi linatumika kwa 6% tu !! Je una maoni gani?

Asilimia 94 ya bomba la gesi haina matumizi linatumika kwa 6% tu !! Je una maoni gani?

0
0

Bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar es salaam ambalo limeigharimu serikali zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.283 imebainika kwa zaidi ya 94% halina kazi.

Kwa mujibu wa report ya CAG inasema Tanesco ndiyo mteja pekee wa gesi ambapo anatumia wastani wa futi za ujazo milioni 46.61 kwa siku ambapo makubaliano yalikuwa ni kutumia futi za ujazo milioni 80 kwa siku. Tanesco ndiyo mteja pekee aliyeunganishwa kwenye bomba hilo na anatumia asilimia sita ingawa gesi ilikusudiwa kuwa na matumizi mengi.

[irp posts=”8634″ name=”Bomba la usafirishaji gesi asilia kati ya Mtwara na Dar es salaam lina udhaifu mkubwa”]

Prof. Assad alisema matumizi ya bomba hilo yapo chini ya kiwango kwa asilimia 94 kwa sababu lilijengwa ili kuwezesha usafirishaji wa gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme, viwandani, kupikia majumbani na kwenye magari. Kiasi hicho ni pungufu futi za ujazo milioni 737.39 kwa siku ili kujaza bomba,” anasema CAG katika ripoti.

Kwa lugha rahisi ni kuwa asilimia 94% ya bomba haitumiki na asilimia 6 tu ndo zinazotumika.

Una maoni gani kuhusu udhaifu wa bomba hili?

Je kwa maoni yako nini kifanyike kuboresha matumizi ya bomba hili ?

[irp]

tags:

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *