Sambaza:

Timu ya Arsenal imeingia kwenye ushirikiano na kampuni ya “Universal Pictures”, kampuni ambayo ni maarufu kwa kuandaa filamu, ushirikiano huu utawezesha wachezaji wa klabu ya Arsenal kuonekana kwenye video za kutangaza filamu mpya zinazotoka hivi karibuni.

Mpango huo utafanya Arsenal kutumika katika kutangaza idadi kubwa ya filamu zinazotolewa na kampuni hiyo, ikiwa ni pamoja na “Despicable Me 3”. Mastaa wa movie ya Replicas – Minions – tayari wamehusika katika shughuli za kufanya matangazo kwenye uwanja wa Emirates, ambapo walisimama uwanjani kabla ya mchezo wa mwisho wa msimu.

“Ushirikiano huu na Illumination na Universal Pictures ni wa kwanza na wa aina yake kwa klabu na tunaufurahi sana,” alisema Vinai Venkatesham, afisa wa biashara wa Arsenal.

“Ni fursa nzuri kwa klabu na studio kutambulishwa kwa watazamaji wapya na tayari tunafanya nao kazi kwa ukaribu kuwatambulisha kwa wafuasi wetu nchini Uingereza na Ireland kuhusu filamu zao zitakazo toka hivi karibuni.”


Wayne Rooney alionekana kwenye promo ya X-Men: Apocalypse

SOMA NA HII:  TANESCO yaanzisha mfumo mpya wa kulipia Bill

Nyota kama Alexis Sanchez na Mesut Ozil wanaweza – kama watabaki Arsenal – pia kushiriki katika trailer za kipekee za filamu.

Arsenal sio timu ya kwanza kukubaliana na ushirikiano kama huo, Manchester United walikuwa na makubaliano na 20th Century Fox hii ilifanya Wayne Rooney aonekane kwenye trailer ya X:Men Apocalypse na mascots  walipaka rangi ya bluu kwajili ya matangazo hayo, ingawa njia hii haikupokelewa vizuri na umma kwa ujumla.

Universal pia imekuwa ikifanya kazi kwenye filamu kuhusu ushindi maarufu wa ligi kwa Arsenal mwaka 1989 huko Anfield.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako