Nyingine

Arsenal au PSG Ni Team Gani Haina Maana? [Toa maoni yako]

Ligi kuu ya mabingwa ulaya raundi ya 16 imekuwa na hekaheka kwa timu zote shiriki. 

Kwa mala nyingine msimu huu Arsenal walicheza na Bayern Munich  na wamepokea kipigo nyumbani na ugenini. The Gunners walipoteza mchezo wa kwanza kwa Bayern inayocheza ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga) matokeo yalikuwa 5-1.

Kwenye mchezo wa marudiano uliofanyika jumanne usiku pale Emirate stadium kipindi cha kwanza vijana wa Arsene Wenger walikuwa sharp katika eneo la ushambulia, hadi dakika 45 zinapoisha walikua wanaongoza  1-0. Ila Bayern Munich walirudi na nguvu mpya na kushusha mvua ya magori baada ya Laurent Koscielny kupewa kadi nyekundu.

Mechi ikaisha 5-1 na kuwaacha mashabiki wa Arsenal wakiwa na majonzi!

Licha ya kufanya vizuri kwenye mechi ya kwanza, PSG wametolewa kwenye Champions league na Barcelona.

PSG walishinda 4-0 kwenye mechi ya kwanza wakiwa nyumbani na maajabu yakatokea pale Camp Nou kwenye mechi ya marudiano walipofungwa 6-1.

Bila shaka, Katika hatua ya 16 bora ya champions league Arsenal na PSG ndo timu zilizopoteza nafasi ya kusonga mbele kwa mtindo wa kipekee.

Kwa kuangalia uwezo wa Arsenal ambayo imefungwa nyumbani na ugenini na PSG ambayo kwa urahisi imepoteza matumaini ya kusonga mbele kuelekea robo fainali.

Ni Team Gani Haina Maana?

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close