Apps bora za Android Kwa ajiri ya Blogger mwaka 2018


Ikiwa wewe ni blogger ambaye unahitaji apps bora ambazo zitakusaidia katika kuendesha blogu yako basi hapa nimeandaa orodha ya Apps bora za Android Kwa ajiri ya Blogger mwaka 2018 ambazo ni muhimu kwa kila blogger. Blogger anaweza kutumia apps hizi ili kufanya maisha yake kuwa rahisi zaidi kuliko hapo awali.

Kila Blogger ndani ya mwaka 2018 anapaswa kujua kuhusu Apps za Android ambazo ni lazima kuwa nazo ili kupata faida zaidi kutoka kwenye simu zao za Android. Programu hizi bora za Android zinakusaidia kutimiza majukumu yako ya kila siku.

Apps-bora-Android-Blogger

Apps 18 bora za Android Kwa ajiri ya Blogger mwaka 2018

1. Whatsapp

Kila mtu anajua kwamba hii ni App bora ya kutumiana ujumbe. Ninatumia app hii kuungana na kushirikiana na Marafiki zangu ambao ni Bloggers kwa kutumia Kikundi cha Waandishi wa Blogu (Bloggers Group).

2. Drippler

Programu hii inanisaidia kujua teknolojia mpya na sasisho za hivi karibuni za teknolojia pia habari kuhusu android. Kupitia app hii unaweza kujua vidokezo vipya, apps, vipengele, sasisho, vifaa na zaidi

3. Dropbox

Kila mara ninapoandika mapitio ya apps za Simu ya Mkono, ninachukua screenshot kwenye simu yangu ya mkononi na kuhifadhi kwenye Dropbox. Inasaidia kufanya kazi yangu kwa haraka bila kuunganisha simu yangu na USB kwenye kompyuta ili kupata picha hizo.

4. Daily Expense Manager

Ninafuatilia matumizi yangu ya kila siku na kila mwezi kwa kutumia app hii. Nafuatilia gharama za kila mwezi za kuendesha blog na vitu vingine vingi kwenye app hii.

5. Buffer app

Mimi nazitangaza makala zangu na blog kwa kutumia Buffer app. App ya Buffer ni app muhimu kwa kila biashara na kwa blogu. Inafanya kazi kwa haraka, rahisi na yenye kufurahisha zaidi.

6. Google Analytics

Nafuatilia Blog traffic kwa kutumia Goole analytics app. Iwapo inahitajika huwa nawaonyesha wateja wangu Analytics za blog yangu ili kufanikisha miradi.

7. Google Keep

Ninaweka taarifa kuhusu kazi zangu za blogu za kila siku na pia kazi zangu nyingine kwa kutumia app hii. Teknolojia ilipofikia hivi sasa hakuna haja ya kuandika kwenye karatasi. Pia natumia app hii kuandika mahitaji ya wateja wangu wakati tunafanya majadiliano.

8. Facebook Page Manager

Facebook Page manager imefanya maisha yangu kuwa mazuri. Hakuna haja ya kufungua akaunti yangu ya facebook ili kushirikisha chapisho langu la blogu. App hii imefanya kazi hiyo kuwa rahisi kwangu na sasa naweza kusimamia kurasa zangu zote 3 kwa urahisi.

9. Pinterest

Ninashirikisha machapisho yangu ya blogu muda wowote ninaotaka kwa kutumia app ya Pinterest na pia napenda kusoma machapisho ya blogu ambayo yamewekwa na wanablogu wenzangu.

10. Quora

Ninakutana na wataalam mbalimbali kwenye Quora. Ikiwa nataka kujua kitu au nataka kupata taarifa zaidi kuhusu mada ninayoandika kwenye blogu yangu daima huwa natafuta kwenye app ya Quora.

11. Skitch

Naipenda sana app hii. Ninachukua screenshots kwenye simu yangu na ninahariri picha, kuweka alama kwa kutumia skitch app ambayo nataka kuionyesha.

12. Twitter

Ninapenda kutweet na kuretweet tweets kutoka kwa wanablogu maarufu. Inasaidia kudumisha uhusiano mzuri. Asante kwa programu ya Twitter.

13. Google Plus

Ninatumia Google plus app kushirikisha chapisho la blogu kwenye Google plus communities ambazo nimejiunga.

14. True Caller

App hii ni ya kushangaza. Ninapenda kuzuia simu kutoka kwa huduma za mitandao ya simu ambazo husumbua sana wakati nafanya kazi zangu muhimu. Ukitumia toleo la premium, itakusaidia kupata namba za simu za wateja wako.

15. Facebook

Facebook app inanisaidia kukutana na wanablogu wenzangu. Pia natumia app hii kutangaza post zangu za blogu na pia kusoma machapisho kutoka kwa vikundi vya blogger.

16. Flipboard

Flipboard ni kama chombo cha kibinafsi cha gazeti. Nimeunda gazeti langu kwenye app hii na pia nimeshirikisha machapisho yangu ya blogu.

17. Google Adsense

Inaonyesha mapato yangu ya sasa na nina uhakika kila mwanablogu anajua app hii ina matumizi gani.

18. Google Drive

Ninapoenda kukutana na wateja wangu mara nyingi natumia Google drive kwenye simu yangu ili kufikia nyaraka zangu na maelezo muhimu. Si lazima kutembea na laptop kila sehemu ninayoenda. Drive app hii ina hifadhi faili zangu zote kwa usalama zaidi na inafanya iwe rahisi kuzipatikana mtandaoni na nje ya mtandao.

Ninapendekeza sana kutumia Apps za Android ambazo ni lazima kuwa nazo kwa kila mwanablogu. Ikiwa kuna baadhi ya app nimezisahau , usisite kuniambia.

Ikiwa Umeona App bora za Android kwa Bloggers mwaka 2018  zina manufaa, Tafadhali washirikishe na marafiki zako na Vikundi vya Whatsapp, Twitter, Google Plus, na Vikundi vya Facebook.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA