Apps 4 za Android Zinazoweza Kukuweka Karibu na Apps na Games Zote Mpya


Watumiaji wengi wa Android wanapenda kuwa karibu na app zote mpya za Android na games zinazo zinduziliwa kwenye soko la Android (Google Play). Lakini, ni vigumu sana kujua kuhusu kila app au game zinazozinduliwa kila siku. Kwa hiyo, leo nimekuja na apps 4 ambazo unaweza kuzitumia kuwa karibu na apps na games zote mpya zinazozinduliwa kwenye soko la Android kila siku.

Apps Bora za Android Unazoweza Kupata Apps & Games Mpya

Sasa tazama app hizi za Android ili upate apps na games bora za Android zinazozinduliwa kila siku:

1. Best Apps Market

BAM (Best Apps Market) ni njia rahisi kabisa ya kupata apps mpya za Android. Inatafuta apps na games mpya na inapendekeza iliyo bora kwako. Inalenga hasa kwenye apps na games za bure.

SOMA NA HII:  Je! Hii inaonekana kama Simu ambayo inaweza kushindana na Apple & Samsung?

Tunaweza kusema kuwa ni njia mbadala na bora ya soko la app za Android lakini kwa uhalisia ni chombo cha kutafuta app kwenye Soko. Inatumia njia ya pekee sana ya kuchuja apps bora kwa kutumia makundi ya aina 100 tofauti.

2. Appreciate

Appreciate ni Soko lako binafsi la App za Android ambayo inakuonyesha apps bora za Android kwa ajili yako tu, kulingana na apps ambazo unazipenda na kuzitumia, na nini marafiki wako wa Facebook, na watumiaji wakubwa wa apps wanapenda na kupendekeza kwajili yako.

Apps za Android

Appreciate ni Android app ya kwanza ambayo ni “fully personalized App Market” Utapata mapendekezo ya apps za kipekee na zinazofaa kwa matumizi yako, na zilizopendekezwa kwa maoni ya watu wanaoendana na wewe.

SOMA NA HII:  Uchambuzi wa simu ya Infinix Hot 5 Lite na Bei yake nchini Tanzania

3. Free Android Market

Free Android Market ni Android app nyingine ya bure ya ambayo inapendekeza kwako mamia ya apps mpya na bora kwenye kifaa chako. Unaweza kushusha apps nzuri, michezo (games), miito ya simu, na wallpapers moja kwa moja kwenye kifaa chako cha Android bila kompyuta!

Ni soko linaloaminika kukuletea apps nzuri zilizofichwa kwenye Google Play kutokana na uwingi wa apps kwenye huduma hiyo na Kutafuta apps ulizotaka kwa sekunde, na kugundua apps bora ambazo hujawahi kuzijua.

4. Free App Market

Free App Market ni soko bora la android ambako utapata games za bure, apps na movie nyingi. Inatoa njia rahisi ya kupata Android apps mpya na zile zinazovuma kwa watumiaji.

SOMA NA HII:  Njia 3 za kuweka App kwenye Android bila kutumia Google Play Store

.App hii inakupa bar ya kutafuta ya kushangaza ambapo unaweza kutafuta apps na utapata matokeo sahihi zaidi.

Kwa hivyo, ikiwa unataka kuwa karibu na apps mpya za Android na games mpya za kuvutia, basi lazima usakinishe (install) moja ya app zilizo orodheshwa hapo juu kwajili ya kifaa chako cha Android .

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA