Apple Wazindua iPad ya Bei Nafuu yenye Kusupport Apple Pencil


Apple imechanganya mambo siku ya Jumanne kwa mkutano wake uliolenga elimu jijini Chicago, Illinois. Mtengenezaji wa iPhone mara nyingi hufanya mikutano yake jijini California, lakini waliamua kutumia Lane Tech College Prep High School kama ukumbi kwajili ya mkutano wake wa hivi karibuni. Na kama ilivyotarajiwa, iPad inazidi kuwa kifaa muhimu zaidi, kwa sababu Apple imezindua toleo jipya, la bei nafuu na uwezo wa kutumia Apple Pencil ambalo litachukua nafasi ya Chromebook kama kifaa kwajili ya wanafunzi.

Licha ya kuwa tablet yake ya bei nafuu hadi sasa, iPad mpya ya inchi 9.7 inaonekana kuwa kifaa chenye nguvu, na ina Retina display, kamera ya megapixel 8, A10 Fusion processor, masaa 10 ya maisha ya betri, GPS, dira na uwezo wa LTE. Inauzwa $ 299 kwa shule, $ 329 kwa watumiaji wengine na inapatikana madukani kuanzia leo.

Mbali na kifaa kipya, Apple pia inaandaa matoleo mapya ya Pages, Numbers na Keynotes apps, ambazo zitakuwa na uwezo wa kutumia Apple Pencil. Apps zote tatu za iWork zitapatikana kwenye iPad mpya bure. Pia, Apple imetangaza kwamba uundaji wa kitabu cha kidigitali unakuja kwenye iPad kupitia Pages app (ambayo, kama Apple ilivyosema, itawekwa kwenye iPads bure), na vitabu hivi vinavyotengenezwa na mtumiaji vinaweza kujumuisha picha, video na michoro inayochorwa kwa Apple Pencil.

Apple pia ilitangaza kuwa hifadhi ya bure ya iCloud kwa wanafunzi imeboreshwa kutoka 5GB hadi 200GB, hii inaongeza nafasi ya ziada kwajili ya kuhifadhi Pages documents na Keynote presentations.

App ya kwanza ambayo Apple ilionyesha kwenye utambulisho wake inaitwa Schoolwork. App hii inawawezesha walimu kuwapa kazi za nyumbani wanafunzi na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi wao. Schoolwork inafanya kazi sambamba na apps zingine kwa kutumia ClassKit API, zote zinaweza kutumika kutengeneza assignments. Schoolwork itaanza kufanya kazi rasmi mwezi Juni

Mwisho, Apple pia ilitangaza third-party accessories ambazo vitakuwa na uwezo wa kufanya kazi na iPad mpya, ikiwa ni pamoja na Crayon stylus ya $ 49, keyboard na vifaa vingine, vyote vimetengenezwa na Logitech.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA