AppsSimu

Apple Music kwajili ya Android sasa imepata usaidizi wa Google

Apple imesasisha (update) app yake ya muziki ya Android baada ya uzinduzi wa iOS 11.

Toleo jipya la Apple Music kwajili ya Android linaruhusu ufanyaji kazi wa  “Google voice assistant” kwenye app hiyo na inaruhusu watumiaji kuunda “profiles” zao ambazo huunganishwa na marafiki ili kuona muziki ambao wanasikiliza. Kipengele hiki kimetolewa kwa watumiaji wa Apple leo.

Apple Music kwajili ya Android sasa pia unakuwezesha kugonga na kushikilia icon ya app hii ili ufikie kwa haraka Beats 1 au ufanye utafutaji.

Toleo jipya la app pia limepokea widget ya kwenye skrini (home screen widget) inayoonyesha muziki wa hivi karibuni, ambapo unaweza kucheza muziki moja kwa moja.

SOMA NA HII:  Razer Simu Janja ya Kwanza (Kutoka Razer) Maalum Kwajili ya Wacheza Magemu
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Toa Maoni Hapa:

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako