Apple kununua app ya kutambua muziki “Shazam”


Apple inakaribia kununua app ya kutambua muziki ya Shazam kwa dola za kimarekani $ 400,000,000, chanzo cha karibu na kampuni hiyo kimeliambia jarida la  Business Insider.

Shazam
CEO wa Shazam. Rich Riley. (Shazam)

Mpango huo utawezesha  Apple kuwa na uwezo wa kuunganisha kipengele hicho maarufu kwa watumiaji wa simu moja kwa moja ndani ya simu zake za iPhones katika kipindi hiki ambapo bidhaa za Apple zinakutana na tishio kubwa kutoka kwa Google na Samsung.

Shazam app inaruhusu watumiaji kutambua muziki unaocheza karibu, kama wimbo katika mgahawa au redioni. Programu hii imekuwa maarufu sana tangu ilipozinduliwa mwaka 2009 na imepakuliwa zaidi ya mara bilioni moja na watumiaji.

Google hivi karibuni imeingiza teknolojia sawa katika simu janja yake ya Pixel 2. Toleo la teknolojia ya Google huangalia muziki wa karibu, kuonyesha jina la kila wimbo kwenye skrini ya simu – kipengele ambacho kinaweza kuwa kimechangia Apple kuhitaji kuwa na teknolojia hiyo kwenye simu zake za iPhones ili kutobaki nyuma.

SOMA NA HII:  MOOVN mfumo wa Teknolojia unaotoa huduma ya usafiri kirahisi na ndivyo hivyo inafanya kazi Tanzania

Mkurugenzi Mtendaji wa Shazam Rich Riley aliiambia Business Insider hapo awali kuwa kampuni ingekuwa na maana kuwa ndani ya kampuni kubwa inayotazamia kuwekeza kwenye muziki au matangazo.

Bei ya dola milioni 400 ambayo Apple inatoa kwa Shazam ni ya chini kuliko hesabu ya hivi karibuni ya thamani ya kampuni hiyo ambayo ni $ 1.02 bilioni, kwa mujibu wa Pitchbook. Hata hivyo, kiwango hicho kinaweza kubadilika kwa mujibu wa mtu wa karibu na mkataba huo aliiambia Business Insider.

Shazam, ambayo ilianzishwa mwaka 1999, ilipata faida ya dola milioni 50 katika mapato ya mwaka jana.

Kampuni hiyo ina makao makuu huko London na imeunda database ya zaidi ya milioni 11 ya “acoustic fingerprints” ambayo huitumia kutambua nyimbo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *