Apple Imetoa Simu Mpya Kuendeleza Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI


Kampuni ya Apple imetoa toleo jipya la simu ya iPhone 8 na iPhone 8 Plus zenye rangi nyekundu, simu zote mbili zina vipengele vya ndani sawa na matoleo ya iPhone 8 na iPhone 8 Plus iliyoyatoa mwaka jana.

Sehemu ya mapato kutoka kwenye mauzo ya simu hiyo yatatolewa kama misaada ya kuendeleza mapambano dhidi ya VVU / UKIMWI.

Katika taarifa yake wiki hii, Apple imesema kupitia mauzo yake ya (PRODUCT) RED imechangia zaidi ya $160 million kwa Global Fund, shirika ambalo linafanya kazi ili kutokomeza UKIMWI. Mbali na iphone, Apple huuza (PRODUCT)RED wireless headphones, iPod Touch, na watchbands kwajili ya Apple Watch.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA