Apple iOSIntaneti

Apple imeonyesha emoji mpya zinazokuja kwenye vifaa vya iOs na macOS

Emoji mpya zipo njiani leo tarehe  17/07/2017 ni siku ya Emoji Duniani.

Je, unatumia bidhaa za Apple? Je, unapenda emoji? Unataka kupata emoji nyingi zaidi? Ikiwa umejibu NDIO kwenye maswali hayo, basi nina habari njema kwako: Apple imetangaza leo kwamba itaongeza emoji mpya ambazo zitatoka na kutumia katika vifaa vya iOs,macOS na watchOS mbeleni mwaka huu. Imeonyesha baadhi ya Emoji mpya katika sherehe ya “Siku ya Emoji Dunia.”

Emoji zitakazoongezwa ni mwanaume mwenye ndevu, mwanamke aliye vaa skafu kichwani, mwanamke anayenyonyesha, Emoji za wanyama na viumbe kama pundamilia na zombi pia Emoji za vyakula kama vile nazi na zinginezo.

Apple hawajasema ni lini emoji mpya zitaanza kutumika, lakini inaonekana kama zitaongezwa kwenye updates za iOS 11 na MacOS High Sierra zitakazotoka hivi karibuni.

SOMA NA HII:  Facebook kufanya utafiti ili kuboresha habari zake
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako