Apple Imeondoa VPN Apps Kwenye China App Store Ambazo husaidia Watumiaji wa Internet Kuepuka Udhibiti


Apps zilizotengenezwa na makampuni ya kigeni kuwasaidia watumiaji wa intaneti nchini China kutumia mitandao iliyofungiwa na nchi hiyo zimefutwa kwenye duka la programu la Apple app store.

Apple Imeondoa VPN Apps Kwenye China App Store

Apple imefuta baadhi ya apps za mtandao wa kibinafsi (virtual private network) kutoka kwenye Apps Store yake nchini China, hatua ambayo inaweza kuzuia uwezo wa watumiaji kupita firewall ya ndani ya mtandao na kuwa na uwezo wa kutumia/kuingia kwenye website za nje ambazo zimezuiliwa nchini humo.

“Tumetakiwa kuondoa baadhi ya apps za VPN nchini China ambazo hazikidhi kanuni/sheria mpya,” Carolyn Wu, msemaji wa Apple nchini China aliiambia Bloomberg kwa njia ya barua pepe, akimaanisha sheria zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari mapema mwaka huu ambayo inawataka watengenezaji wote wa VPN kupata idhini ya serikali.

VPN ni maarufu nchini China kwa kuwasaidia watumiaji kupita Great Firewall, mfumo unaotumiwa na China kudhibiti ufikiaji wa mtandao. Kuondolewa ni ishara ya hivi karibuni ya hatua za China kuimarisha kuzuia watu kuingia kwenye mitandao ya kibinafsi,kufuatia kufungwa kwa huduma kadhaa maarufu za VPN.

Wu alisema app za VPN zinaendelea kupatikana katika masoko mengine yote ambayo Apple inafanya biashara.

MIIT ya China haikujibu mara moja faksi ya Bloomberg kutoa maoni yao juu ya suala hilo.

Ningependa kusikia kutoka kwako, je mpango wa China kupambana na matumizi ya intaneti kwa mtazamo wako una manufaa ? je mfumo kama huu ukitumiwa na serikali ya Tanzania utakuwa na manufaa ? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku Kwa Sababu Tunaaminika Katika Teknolojia.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA