Sambaza:

Imeripotiwa kuwa Amazon.com inataka kuzindua programu yake ya ujumbe inayoitwa Anytime, kwa mujibu wa ripoti kutoka AFTV News.

Kampuni hiyo kubwa mtandaoni inayojihushisha na biashara ya kuuza na kununua bidhaa katika mtando imeanza kufanya tafiti kwa wateja wake juu ya vipengele muhimu vya mtandao huo, ingawa haijulikani bidhaa ya mwisho itakuwa ya aina gani.

App hii itakuwa na vipengele vyote muhimu ambapo inaweza hata kushindana na mitandao ya kijamii kama vile Facebook Messenger, WhatsApp na zingine.,” huku msisitizo ukiwa umewekwa kwenye kutuma na kupokea meseji za kawaida, simu za video na sauti, ku’share picha.

Picha: AFTV News

Watumiaji watakuwa na uwezo wa kuweka ‘filter’ katika picha zao au video, @mention watumiaji wengine, kutumia “sticker” na mfumo wa GIF, pia kucheza michezo mbalimbali (games).

SOMA NA HII:  Orodha ya njia za mkato za keyboard katika Mozilla Firefox

Pia watumiaji wataweza kuwapigia (sauti na video) watu wengine au vikundi, kufanya mawasiliana ya kibiashara ili kuagiza bidhaa.

Kwa mujibu wa picha zilizochukuliwa kutoka kwenye utafiti huo, huduma hiyo itakuwa salama na itafanya kazi kwenye vifaa mbalimbali vya desktop na vifaa vya simu.

Je wewe Amazon unawapa maksi ngapi ? Niandikie maoni yako hapo chini sehemu ya comment.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako