Ilichukua miezi tisa kwa Duo app ya Google ya ku-stream video kufikisha downloads milioni 50 za kwanza. Imechukua miezi miwili tu kufikia downloads milioni 50 zingine, na hivi sasa Duo imewekwa kwenye simu zaidi ya milioni 100.

Ingawa hakuna takwimu ambazo zinatuambia mara ngapi Duo inatumika, Google imerahisisha matumizi ya Duo. Mwezi machi mwaka huu Google ilitoa toleo jipya linalo kuruhusu “audio calls” kwenye Duo. Hii inafanya programu hii kuwa muhimu zaidi.

Pengine jambo muhimu zaidi ambalo limechangia kuongezeka kwa watumiaji wa Duo ni kutokana na ukweli kwamba kuanzia Desemba mwaka jana, Duo ilianza kuweka kwenye simu mpya za Android kama sehemu ya programu za simu hizo. Hizi bado huhesabiwa kama “installation”  hata kama hazijawahi kuwa “activated” au zimeondolewa.

SOMA NA HII:  Google itahamasisha wafanyakazi 10,000 kuboresha video za YouTube

Duo hufanya kazi kwenye Android na iOS huku FaceTime ikiwa kwajili ya iOS tu. Uwezo wa jukwaa hili inamaanisha kama mtu anamiliki bidhaa ya iOS na anahitaji kuzungumza na rafiki zake wanaotumia Android kwa njia video , au kinyume chake, Duo ni programu pekee inayohitajika.

Amit Fulay, ambaye ni mkuu wa bidhaa wa Allo na Duo, Amesambaza tweet akisema kuwa programu imepakuliwa mara milioni 100 katika miezi 11, na kwamba kuna “mambo mengi zaidi ya kufanya.”

Kitu kilichokosekana kwenye taarifa ya wiki  hii ni habari kuhusu watumiaji wa kila mwezi. Hadi Google itakapotoa taarifa hiyo, ndio tutajua jinsi Duo inavyofanya vizuri.

SOMA NA HII:  Wanafunzi wa Primary Tanga kuanza kusoma kwa kutumia Tablet

Unaweza kupakua App hii kwa kubonyeza hapa (Android|iOS).

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako