Habari za Teknolojia

Unapenda Muziki ? Hizi Ni App 5 Za Android Kwajili Ya Kupakua (download) Muziki

Hebu waza maisha bila muziki. Kuishi bila muziki unaotuliwaza, bila muziki wa kimahaba, bila nyimbo za kisasa zenye midundo yenye kuvutia.? Muziki una sehemu kubwa sana katika maisha yetu.

 

Simu zetu zimechukua nafasi kubwa kama chombo cha kusikiliza muziki kuliko redio na hata vifaa spesho vya kucheza muziki maarufu kama vile iPod.

Karibia kila simu janja ina uwezo wa kuunganisha na intaneti au hata WiFi. Sasa kama simu yako inaweza ikaingia katika intanenti basi unaweza kabisa ukashusha nyimbo nyingi kadri kifaa chako kinavyoweza kupokea.

Hapa nakusogezea App Bora kwa ajili ya kushusha Muziki katika simu janja yako ya Android.

4shared Music

4Shared-Music

 

Hii ni App spesheli ambayo imeandaliwa kwa wale wanaopenda muziki. Ndani ya App hii kuna kipengele cha ‘Tafuta’ (Search) ambapo mtu unaweza tafuta muziki unaoutaka na kuuweka katika ‘PlayList’ katika ‘4shared Music’. Pia unaweza ukatengeneza ‘PlayList’ yako mwenyewe na unaweza hata kupandisha miziki kutoka katika simu yako kwenda katika App hii. App hii inatoa GB 15 za bure ambazo mtumiaji anaweza akahifadhi miziki mingi katika App hii.

RockMyRun

RockMyRun

 

Hii app ni spesheli kwa wale ambao wanafanya mazoezi (hasa hasa asubuhi). App hii itakusaidia sana katika kufanya mazoezi kwa sababu inajulikana kama moja kati ya App nzuri zaidi za Mp3. Na pia App hii inafanya kazi na  ma’DJ wakali ambao wanatengeneza Mix kali kabisa ambazo zinaendana na mazoezi ya mwili.

SOMA NA HII:  Drones kutumika kuwafukuza wafanyakazi kazini

 

Anghami

Anghami

 

Hii ni moja kati ya app za Bure ambayo inahusisha kushusha muziki katika simu zote za Android. Kwa kutumia App hii unaweza kushusha mamilioni ya nyimbo duniani katika kifaa chako cha Android.

Wynk

Wynk

 

Hii ni app ya kushusha miziki katika kifaa cha Android ambayo ina zaidi ya miziki milioni 1.8. Kwa haraka unaweza ukaishusha miziki hiyo au kuisikiliza bila kuishusha (Stream).

Sound Cloud

Soundcloud

 

App hii ni nzuri na inatumiwa sana kwa wapenda muziki na hata wanamuziki wanaochipukia. Ina mamilioni ya watumiaji, kwa kutumia App hii unaweza ukashusha muziki unaoutaka baada ya kuutafuta ndani ya App. Pia unaweza ukacheza muziki bila kuushusha (Stream) ndani ya App. Pia unaweza ukawafollow marafiki na kujua ni miziki gani wanasikiliza.

Niambie katika App hizo ni ipi ambayo unaipenda sana ?

Toa maoni yako.

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako