Nyingine

Anna Mghwira: Siioni Tanzania ya uchaguzi mwaka 2020, hatuna chaguzi za demokrasia

on

Jumatatu ya tarehe 17 Aprili 2017 kwenye kipindi Cha Dakika 45 cha ITV aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama cha siasa ACT – Wazalendo, Anna Mghwira amedai Tanzania bado haina uchaguzi wa demokrasia huku akiweka wazi mpango wake wa kugombea ubunge katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020 jimbo la Singida.

“Siwazi siioni Tanzania ya uchaguzi ya mwaka 2020. Hatuna chaguzi za demokrasia bado. Pengine naweza kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Singida mjini mwaka 2020,” alijibu Mama Anna Mghwira wakati akieleza mipango yake katika uchaguzi ujao.

Mama Anna Mghwira pia ameishauri serikali kuwekeza katika kilimo ili kuiandaa Tanzania ya Viwanda.

“Hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda bila ya kuboresha kilimo kwanza, Tunahitaji kuwa na Tanzania ya kilimo kwanza,” .

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Reply

Your email address will not be published.