Simu za Mkononi

Angalia Simu ya Kwanza Duniani yenye Mtandao wa 5G (Picha)

Mtandao wa 5G? Makampuni mengi ya kutengeneza simu tayari yanavutiwa na wazo hili. Wachambuzi wengi wametabiri kwamba mtandao huu wa kizazi cha 5 (5G) utapatikana ifikapo mwaka wa 2020 na Qualcomm kampuni kubwa ya smartphone inafanya kazi kwa bidii ili kufanikisha wazo hili.

Je 5G ni nini?

5G ni teknolojia ya wireless broadband ya kizazi cha tano yenye kiwango cha IEEE 802.11ac. Teknolojia ambazo zitatumika katika 5G bado zinaelezewa.

Hasa, mitandao ya 5G itatumia aina ya encoding inayoitwa OFDM, sawa na ile inayotumiwa katika 4G LTE, na mitandao ya 5G itakuwa midogo sana na ya kisasa zaidi, ikilinganishwa na mifumo yote ya awali.

Ufafanuzi wa mtandao wa 5G:

International Telecommunication Union (ITU) imetoa maelezo yafuatayo kuhusu kizazi cha tano cha mitandao ya simu. Uwezo wa jumla wa kupakua kwa simu ya mkononi ya 5G lazima iwe angalau 20Gbps.

Kiwango cha 5G kinachokuja kitakuwa na uwezo wa kuunganisha vifaa milioni 1 kwa kilomita ya mraba

Kiwango hicho kitahitaji “carriers” kuwa na angalau 100 MHz za ziada, hadi 1GHz kama inawezekana.

Simu ya Mkono ya 5G ni nini ? Mtumiaji wa Twitter aitwaye Sherif Hanna alishirikisha picha ya smartphone ya kwanza ya 5G dunia. Yeye pia ni Marketing Lead wa LTE na 5G NR Modems za Qualcomm.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno Phantom 6 Plus bei na Sifa zake

Tweet yake inasema – “Ngumu kuamini kwamba nina smartphone ya kwanza ya 5G mkononi mwangu!”

Kwa mujibu wa Digit, picha hiyo kimsingi ni ya mfano wa simu ya kwanza ya 5G ya Qualcomm na sio simu halisi kwa sababu bado ipo kwenye hatua za mwanzo za kutengenezwa. Smartphone hii imewekwa maalum ili kupima na kufanya uboreshaji muhimu wa utendaji wa 5G mmWave.

5G sio tu itawezesha matumizi mazuri ya simu za mkononi, lakini pia itaanzisha zama za magari yasiyo na dereva na smart homes.

Wakati wa Mkutano wa Qualcomm 4G / 5G wa mwaka 2017, walitangaza Qualcomm Snapdragon X50 5G modem na waliweza kufikia uhusiano wa data wa 5G kwenye chipset ya modem ya 5G kwa vifaa vya simu.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako