Angalia Ndege aliyezaliwa na Miguu minne huko Brazil

Comment

Kuku amezaliwa nchini Brazil akiwa na miguu minne. Ndege huyo, ambaye ametotolewa shambani amewashangaza watu na wanabiolojia wa eneo hilo na kuwaacha bila ya kuwa na majibu, ila kuku huyo ana furaha na kuwa na miguu minne hakujamuathiri chochote. Video inayoonyesha kifaranga hicho cha kuku kikitembea na miguu yote minne imesambaa mtandaoni na kifaranga hicho hakionyeshi kupata shida yoyote kutembea na miguu minne.

Sababu ya kifaranga hicho kuzaliwa na miguu minne bado haijafahamika na wanabiolojia bado wanatafuta majibu, kwa sasa kifaranga hicho kimepewa jina la “franken-chicken.”

Angalia video hapa chini:

Up Next

Related Posts

Discussion about this post

error: Content is protected !!