Nyingine

Angalia kikosi cha Yanga kitachoenda kupambana na Alger

Klabu ya soka ya Yanga SC inapenda kutoa taarifa juu ya safari yake leo Alhamisi kwenda Algeria katika mechi ya marudiano dhidi ya Mc Alger.

Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka Alhamisi jioni majira ya saa 12 kwa ndege ya shirika la Emirate kupitia Dubai.

Wachezaji watakaondoka ni Makipa: Deogratius Munishi na Beno Kakolanya.

Nafasi ya ulinzi: Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua, Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani.

Viungo: Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke, Said Makapu, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geoffrey Mwashiuya na Emmanuel Martin.

Upande wa washambuliaji ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma.

Wachezaji wafuatao wataukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali Justine Zulu, Malimi Busungu, Matheo Antony, Ally Mustapha, Pato Ngonyani, Obrey Chirwa na Yusuph Mhilu.

Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano
Young Africans SC
12/04/2017.

SOMA NA HII:  Kuwa mkweli! Jina gani umetumia ku-save namba ya simu ya mama yako?

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.