Android Go Edition: Toleo la Android Kwa Simu za Hali ya Chini


Android Go ni toleo spesheli la mfumo endeshi wa Android kwa simu zenye ukubwa wa RAM 1GB au chini ya hapo, yaani simu janja zenye uwezo mdogo. Toleo la sasa limesanifiwa kutoka kwenye Android Oreo (Go Edition), ila hili halihitaji nguvu kubwa ya simu ili kuweza kufanya kazi katika utendaji unaoridhisha.

Kupitia Blog ya Habari ya Google imesema imeamua kutoa Toleo la Android Go ambalo litaweza kusupport programu za sasa ili kutimiza lengo la kuzalisha simu janja za bei rahisi kununuliwa na watu wa hali ya chini.

”Mwaka jana tulianzisha Android Oreo (Go Edition), toleo la Android Oreo lililopendekezwa kwa simu za mkononi za chini ya 1GB ya RAM na kwa kiasi kidogo cha uhifadhi na nguvu za utunzaji umeme, simu hizi ni za gharama nafuu kwa wazalishaji na zinaweza kuuzwa kwa bei nafuu, wakati mwingine hata kufikia chini ya dola 50.”

Android Go itaweza kufanya kazi kama Toleo la Android Oreo ambayo itaweza kusaidia programu za kisasa kujiendesha vizuri tofauti na Matoleo yaliyopita.

Muonekano wa simu yenye Android Go

Hii imefanywa hivi kwa kuwa Mifumo endeshi ya Android ya nyuma kwa sasa imekuwa haiendani na App nyingi na Mifumo ya Android ya sasa ni yenye kula nafasi kubwa na yenye kuhitaji simu iwe na kiasi kikubwa cha RAM hususani kuanzia RAM 2GB na kuendelea.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA