Nyingine

Alikiba: Nimewaambia Sony Music wasiwaangushe mashabiki wangu tena

Alikiba akiwa na CEO wa Sony Music Africa, Sean Watson

Alikiba yupo nchini Afrika Kusini kwaajili ya ziara yake kubwa, kupitia mahojiana aliyofanya nchini humo Kiba amesema ameyasikia malalamiko ya mashabiki wake kuhusu ukimya wake.

Kutokana na ukweli huo, Alikiba amelazimika kuwaambia mabosi wa Sony kuwa wajipange vyema ili kuhakikisha kuwa mashabiki wake wanaridhika.

Kwenye interview na millardayo.com, Alikiba amesema:

CEO wa Sony Music Africa, Sean Watson, ameiambia bodi ya label hiyo jinsi Alikiba alivyo na mashabiki wengi nyuma ambao panapotokea kuchelewa kwa lolote, ‘hung’ata kama nyuki.’

“Kwahivyo they have to make sure kila kitu kinaenda on point, kila kitu hakitakiwi kudelay, kila kitu kinakwenda sawa,” .

“Yaani they have to make sure kwamba hawadisappoint fans wangu, kwasababu pressure ambayo wanapata yaani tayari Sean ameelewa kwahiyo wamekubali wamesema sawa, nadhani fans kitu hicho sasa nimekiacha mikononi mwa jamaa na kama kutakuwa na chochote mtakuwa mnapeleka malalamiko yenu kwao,” amesisitiza.

Zinazohusiana

1 thought on “Alikiba: Nimewaambia Sony Music wasiwaangushe mashabiki wangu tena”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *