Home Nyingine Alikiba: “Kutoa nyimbo nyingi ni kutojiamini”

Alikiba: “Kutoa nyimbo nyingi ni kutojiamini”

0
0

Hitmaker wa Mwana, Alikiba amedai yeye anaamini kutoa nyimbo mara kwa mara ni kutokujiani na ufujaji wa kipaji

Muimbaji huyo ambaye amekuwa akishinikizwa na mashabiki wake kuachia wimbo mpya ikiwa ni miezi kadhaa toka aachie video ya wimbo ‘Cheketua’, alikiambia kipindi cha The Sporah Show cha Clouds TV kuwa yeye akitoa kazi yake moja ina uwezo wa kukaa sokoni kwa muda mrefu.

“Fans don’t worry about me, kitu ambacho nafanya ‘New Kiba New Year’ ni kutaka kwenda sawa na nyie. Lakini nilikua nataka mnielewe kutoa nyimbo kila dakika ni umalizaji wa talent yako au kutokujiamini au talent yako fupi au una jaribu. Mimi najiamini kwa kitu ambacho natoa na ni muda gani natakiwa kurudi tena,” alisema.

Aidha, Alikiba aliwataka watu kuacha kumfananisha na wasanii wengine kwakuwa yeye anafanya vitu tofauti na wengine.

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *