Home Nyingine Alichoandika Nay wa Mitego kuhusu Vanessa Mdee na sakata la dawa za kulevya

Alichoandika Nay wa Mitego kuhusu Vanessa Mdee na sakata la dawa za kulevya

0
0

Muimbaji Vanessa Mdee alijisalimisha kwa jeshi la polisi siku 5 zilizopita baada ya kutajwa kwenye list ya RC Makonda ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kutakiwa kujisalimisha polisi central kwajili ya mahojiano.

Rapper Nay wa Mitego ameonyesha kuguswa na tukio hilo lililomtokea muimbaji huyo maarufu huku akimtaka kuvumilia kwa yote yanayoendelea. Kupitia ukurasa wake wa Instagram,Nay ameandika:

Vanessamdee Sijui ulipo anzia, but mpaka apa ulipofikia umepambana sana. Nina imani mungu ndo aliye kufanyia wepesi mpaka kua #BrandKubwa na kupata hatua Ulizo nazo. Naamini Mungu Huyu Huyu ndiye atakae kufanyia Wepesi Kwenye yanayo kukabili ivi sasa. Amini izi ni Changa moto tu na ni Mapito ambayo Binadamu tunapitia kwenye Safari ya kuelekea kutimiza Ndoto zetu.

Aliongeza, “I pray for you my friend Vanessa, naamini brand yako haiwezi haribika kirahisi kwa sababu umepambana sana ni wasichana wachache wenye kuweza ku-fight kama wewe. Mungu ata kusimamia uzidi kusonga mbele, Haya yata pita nina imani utakua strongZaidi. #CashMadame KeepItUp. Napenda kuona Wasichana wakifanikiwa kwa kufanya kazi kwa bidii #VannesaTheBrand wewe ni mwanamke wa shoka. Usiyumbishwe kuwa Mfano. Najivunia uwepo wako kwenye Game,

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *