Akismet ni Nini na Kwa Nini Unatakiwa Kuitumia Kwenye Tovuti Yako


Kila WordPress installation Inakuja na Plugins mbili zilizowekwa kabla (pre-installed). Moja wapo ni Akismet, ambayo ni dhahiri ipo katika orodha yetu ya Plugins muhimu za WordPress. Ingawa Akismet unakuta tayari imewekwa, inakuwa bado haijaamilishwa (not activated). Unatakiwa kuchukua hatua za ziada ili kuifungua (activate). Katika makala hii, tutaelezea Akismet ni nini na kwa nini unapaswa kuanza kuitumia kwanzia sasa. Pia tutakuonyesha jinsi ya kufanya setup ya Akismet kwenye tovuti yako ya WordPress.

Akismet ni nini?

Akismet ni huduma ya kuchuja spam kwenye maoni (comment spam filtering service). Jina lake Akismet linatokana na Automattic na Kismet. Auttomatic ni kampuni inayosimamia Akismet, na ilianzishwa na mwanzilishi wa WordPress Matt Mullenweg. Akismet huchukua maoni ya blog na ku-pingback spam kwa kutumia algorithms zao. Algorithms hii inajifunza kutokana na makosa yake na kutoka kwa hatua zilizochukuliwa na tovuti zinazoshiriki. Kwa mfano, wakati tovuti kadhaa zinaanza kutoa taarifa kwamba maudhui fulani ni spam, basi Akismet itajifunza kutambua aina hiyo ya maudhui kama SPAM katika siku zijazo.

Kwa nini unapaswa kutumia Akismet?

Kwenye tovuti maarufu, kiasi cha maoni ambayo ni spam kinaweza kufikia hadi 85%. Hii inamaanisha katika kila maoni 100, maoni 15 tu ndio halali. Kupima maoni (Comment moderation) ni kazi inayotumia muda mwingi, na Akismet inaweza kuokoa masaa yako. Akismet itakamata spam comments kabla ya kuingia kwenye moderation queue kama pending. Hii inakuwezesha kuzingatia zaidi maoni ya watumiaji halisi.

Malalamiko ya Watumiaji

Zamani watumiaji waliikosoa sana Akismet kwa kutoa false positives. False positives ni maoni halali ambayo huchukuliwa kama spam na Akismet. Hii inaweza kutokea kwa sababu mbalimbali. Moja ya sababu ya kawaida ni kama maoni ya mtumiaji fulani yamewekwa kama spam na blogu kadhaa, basi Akismet itasoma maoni yote ya mtumiaji huyo kama spam. Kama automated platform zingine , Akismet haipo kamili, lakini ni bora zaidi.

Jinsi ya kujua kama Maoni yako yaligunduliwa kama Spam

Ikiwa maoni yako yalitambuliwa kuwa spam na Akismet, basi hutaona taarifa ya kupima maoni (Awaiting Moderation notice) kama unavyoona kwenye maoni ya kawaida. Ikiwa unawasilisha maoni kwenye tovuti, na huoni maoni yako yakiwa pamoja na taarifa inayosema awaiting moderation, basi unapaswa kuwasiliana na msimamizi wa tovuti mara moja. Wanaweza kusaidia kutoa maoni yako nje ya sanduku la spam, na baada ya muda Akismet itajifunza kutokana na makosa yake.

 Jinsi ya Kuanza Kutumia Akismet katika WordPress

Jambo la kwanza unatakiwa kufanya ni kwenda kwenye Plugins na kisha activate Akismet.

Baada ya kuwezesha, Akismet inaongeza kitu kipya kwenye menu katika Plugins » Akismet Configuration. Bonyeza kwenye Akismet Configuration itakupeleka kwenye skrini ya Akismet Configuration. Kwenye ukurasa huu, utatakiwa kuingia Akismet API Key yako. Ondoka kwenye huo ukurasa na fungua sehemu mpya ya kivinjari. Tutarudi kwenye ukurasa huu baada ya kuunda API key ya Akismet.

 Jinsi ya Kupata API Key ya Akismet

Ili kuwezesha Akismet kwenye tovuti yako, unatakiwa kuwa na API Key. Nenda kwenye tovuti ya Akismet na bonyeza kwenye Get a WordPress Key .

Hii itakupeleka kwenye mipango ya Akismet na ukurasa wa bei. Akismet ni bure kwa tovuti binafsi na zisizo za biashara Kwa tovuti za biashara, kuna mipango na vifurushi tofauti. Chagua chaguo linalokufaa zaidi. Bila kujali mpango gani umechagua hatua zilizobaki zitakuwa sawa. Bofya kwenye sehemu ya Sign up ili kuendelea.

Kwa kubonyeza Sign up itakupeleka kwenye skrini inayofuata ambapo utatakiwa kujiandikisha na WordPress.com. WordPress.com ni huduma ya blog hosting kutoka Automattic, kampuni ambayo inakuletea Akismet. Hata hivyo, WordPress.com si sawa na tovuti yako ya WordPress.org. Kwa habari zaidi, angalia Self Hosted WordPress.org dhidi ya Free WordPress.com  na Jinsi WordPress.com na WordPress.org zinavyohusiana. Unaweza kuunda akaunti ya WordPress.com bila kuunda blogu. Bonyeza kwenye Sign up with WordPress.com ili kuendelee. Hii itafungua fomu rahisi ya kujiunga.

Ikiwa tayari una akaunti ya WordPress.com, unaweza kubofya link ya I already have a WordPress.com account. Ikiwa huna akaunti ya WordPress.com, basi kujaza maelezo na kuunda moja.

Mara baada ya uthibitisho na WordPress.com kukamilika, utarejeshwa kwenye tovuti ya Akismet. Huko utatakiwa kutoa maelezo ya mtumiaji pamoja na maelezo ya malipo. Ikiwa umechagua mpango wa bure, basi rudisha kiasi cha bei hadi $ 0.

Bonyeza sehemu ya continue na utapelekwa kwenye skrini inayoonyesha API key yako. Pia utapokea barua pepe kutoka Akismet iliyo na API Key yako.

Kumbuka, API key ni kama nenosiri. Usimtajie mtu yeyote. Ikiwa umepoteza au kusahau API key yako, unaweza kutembelea Akismet.com na bofya kwenye sehemu ya sign in kuingia kwenye ukurasa wako wa akaunti. Baada ya kuingia utaona Akismet API key imefichwa. Bonyeza Kwenye Reveal link ili kuona API key yako.

 Kutumia Akismet API Key katika WordPress

Nakili Akismet API key yako na urejee kwenye sehemu ya admin ya tovuti yako ya WordPress. Nenda kwenye Plugins »Akismet Configuration na kisha paste API Key. Chaguzi zingine kwenye skrini hii ni chaguo binafsi. Mara baada ya kubonyeza Update Options, Akismet sasa itahakikisha key yako na kukuonyesha ujumbe wa mafanikio:

Kuonyesha Takwimu za Akismet kwenye Tovuti yako

Baada ya kuingia kwenye tovuti yako ya WordPress, utaona maelezo ya jumla ya Takwimu za Akismet. Itakuonyesha idadi ya maoni ya Spam yaliyopatikana na Akismet, na yapo mangapi katika  spam queue yao mpaka sasa. Inashauriwa sana uangalie spam queue yako mara kwa mara ili usikose maoni halali yanayofutwa kwa makosa.

Kuna mtazamo wa kina wa takwimu za Akismat unapatikana kwenye menyu ya Dashboard » Akismat Stats. Bofya hapo itakuonyesha takwimu za kina za spam na ham comments kwenye tovuti yako. Pia unaweza kuona idadi ya maoni yaliyokutwa na Akismet ambayo ni spam.

Ikiwa unataka kuonyesha idadi ya spam comments ambazo Akismet imezikamata kwenye tovuti yako, basi unaweza kutumia Akismet Widget. Nenda Appearance » Widgets, drag and drop Akismet Widget kwenye sidebar yako.

Tunatarajia makala hii imekusaidia kuwezesha Akismet kwenye tovuti yako, kupata Akismet API Key na kujifunza kwa nini Akismet ni muhimu. Spam comments ni suala kubwa linalozikabili tovuti nyingi za WordPress. Jinsi tovuti yako inavyokua, utagundua kwamba unahitaji chaguzi nyingine za kufanya kazi pamoja na Akismet ili kupunguza kiasi cha spam. Kwa mfano, unaweza kuzuia spam comment bots katika WordPress na honeypot. Kwa kuwa spammers wengi wanapenda kuweka spam links kwenye tovuti yako, unaweza kuondoa sehemu ya URL kwenye fomu ya maoni ya WordPress kama tulivyofanya. Pia tumejumuisha orodha ya vidokezo na zana za kupambana na spam  kwenye maoni katika WordPress. Kwa maswali na maoni tafadhali toa maoni yako hapa chini.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA