AJALI ARUSHA: Watu wengine watano wamefariki Arusha wakiwa ndani ya nyumba

Watu watano wamefariki dunia mkoani Arusha ikiwa bado Watanzania wapo kwenye majonzi ya msiba wa watu 32 kwenye ajali ya basi dogo la shule Karatu Arusha.

Watu hawa watano wamefariki baada ya kuangukiwa na mti kwenye kijiji cha Ngiresi kilichopo Kata ya Sokoni mkoani Arusha.

Kamanda wa Polisi Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, amesema imetokea usiku wa kuamkia leo May 9, 2017 baada ya mti kuangukia kwenye nyumba iliyokua jirani ambapo chanzo ni mvua na upepo mkali.

Leave a Reply