Biashara Mtandaoni

Airtel ni mali ya TTCL Palifanyika Mchezo wa Hovyo – Rais John Magufuli

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Fedha kufuatilia kwa karibu suala la umiliki wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel, akidai kwamba kwa taarifa alizonazo Airtel Tanzania ni mali ya TTCL Tanzania kwa asilimia miamoja.

“Kuna michezo michafu sana inaendela…hakikisha unafuatilia suala hili kabla ya mwaka huu kuisha, alisema Rais Magufuli wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi la ofisi ya taifa ya takwimu Dodoma.

Katika hafla hiyo Rais Magufuli alitoa onyo kwa wale ambao wanakuja na takwimu zao za mifukoni na kuzitaka mamlaka husika kutumia sheria zilizopo kuwabana wale ambao wanataka kuwapotosha Watanzania kwa takwimu zao za uongo. “Ukikosea kutoa takwimu…umeichafua nchi,” alisema Rais Magufuli.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.