Air Namibia Inakuwa Kampuni Ya Ndege Ya Sita Kutoka Afrika Kuwa Na Ruhusa Ya Kuingia Marekani


Shirika la ndege linalomilikiwa na Serikali ya Namibia ,”Air Namibia” limepewa kibali kuruka ndani na nje ya Marekani, jambo hili limefanya shirika hilo kujiunga na safu ya kipekee ya mashirika ya ndege kutoka barani Afrika yenye ruhusa ya kufanya hivyo.

Air Namibia sasa inaruhusiwa kuruka nchini Marekani. Photo: airnamibia.com

Hapo awali,shirika la South African Airways, Ethiopian Airlines, Egypt Air, Moroccan Royal Air Maroc na Cape Verde’s TACV airline pekee ndiyo yalifurahia haki ya kusafirisha abiria ndani na nje ya Marekani kutoka Afrika.

Kampuni hii ambayo imekuwa ikipata hasara kwa muda mrefu inatarajia kuzalisha mapato kupitia mikataba yake “codesharing” na washirika wake nchini Marekani, pamoja na ruhusa yao mpya ya kuruka katika nchi yoyote iliyomo kwenye umoja wa Ulaya,kwa mujibu wa CNBCAfrica.

SOMA NA HII:  Ripoti : Idadi ya watumiaji wa Intaneti yaongezeka Kufikia milioni 23

Mkurugenzi mtendaji wa Air Namibia , Mandi Samson, alisema shirika hilo la ndege limepata kibali cha kusafiri nje ya Afrika mwezi Aprili, na sasa kibali cha U.S. kitaruhusu kampuni hiyo kuongeza mauzo ya tiketi kwa njia ya mashirika ya ndege ambayo wameingia kwenye ushirikiano.

Ripoti ya UK-Oxford Economics imekadiria kwamba kwa mwaka 2020/21, idadi ya wageni wanaosafiri kupitia Air Namibia itakuwa zaidi ya 230,000.

Ripoti inaonyesha kwamba mchango wa kiuchumi kutokana matumizi ya wageni unatarajiwa kukua kwa karibu $ milioni 129, kuendeleza ajira 7,700 katika uchumi wa Namibia na kuongeza zaidi ya $ milioni 33 katika mapato ya kodi, kwa mujibu wa NewsGhana.

SOMA NA HII:  Selfie yamsababishia Mwanamke kifo….Akifurahia maisha.

Katika mwaka 2015/16 mchango ya ndege katika uchumi ulifikia zaidi ya $ milioni 53, ripoti inaonyesha.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA