Home Nyingine Ahmad Ahmad wa Madagascar ampiga chini Hayatou urais wa CAF

Ahmad Ahmad wa Madagascar ampiga chini Hayatou urais wa CAF

0
0

Hatimaye Rais wa chama cha soka cha Madagascar Ahmad Ahmad aamefanikiwa kumbwaga Issa Hayatou ambaye alikuwa rais wa muda mrefu wa shirikisho la soka Afrika na kushinda urais wa Caf leo March 16, 2017.

Uchaguzi uliomalizika Addis Ababa umempa ushindi Ahmad Ahmad baada ya kupata kura 30 dhidi ya 20 za Issa Hayatou.

Hayatou alikalia kiti hicho cha urais kuanzia Machi 10 mwaka 1988 ikiwa ni takribani miaka 29.

Ahmad anakuwa rais wa saba wa CAF kwenye historia ya shirikisho hilo lenye miaka 60 hadi sasa tangu kuanzishwa kwakwe.

Wakati huo huo ombi la Zanzibar kuwa mwanachama mpya wa shirikisho hilo limepitishwa bila kupingwa na kufanya jumla ya wanachama kwenye shirikisho hilo kufikia 55 mpaka sasa.

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *