BiasharaProgramu

AcuteInvoice Inataka Kukusaidia Kuandaa Ankara Zako Za Malipo

Ikiwa una mauzo ya juu sana, kuna kila uwezekano wa kuwa hauwezi kufuatilia malipo na bila shaka kama biashara yako haijabadilika, unaweza kuwa unatumia njia za kawaida za malipo kwa wateja wako. Ikiwa ndivyo ilivyo kwa upande wako, usishangae ikiwa wateja wako hawafanyi malipo haraka iwezekanavyo.

Ukweli ni kuwa unahitaji programu ya malipo ambayo itakusaidia kuandaa ankara zako.

Hivyo ni jukwaa gani la malipo ambalo unatumia? hapa, tunapendekeza AcuteInvoice. AcuteInvoice inakuwezesha kurudia kwa urahisi na kurekebisha ankara zako zilizopo. Ni njia inayojitosheleza ya kuendesha mfumo wa ankara zako mtandaoni. Wateja wako wanaweza kubofya kulipa ankara na malipo kuingia katika akaunti yako ya benki mara moja.

Unaweza kuongeza alama yako ya biashara (business logo), maelezo ya kibinafsi, maelezo ya malipo na hata kurekebisha rangi za ankara ili zifanane na brand yako.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kufungua Akaunti ya Paypal nchini Tanzania
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.