Sambaza:

Unaikumbuka laptop  kwajili  ya kucheza gemu Acer Predator 21 X ? kwa wasiokumbuka, laptop hii ilikuwa inauzwa $8,999!

Ndio.

Sasa, Acer wametoa laptop nyingine— Nitro 5— kwajili ya watu ambao hawawezi kulipia $8,999. Wazo kuu ni kutengeneza kompyuta ndogo yenye uwezo wa kucheza gemu zako kubwa lakini kwa bei ya kawaida.

Tofauti na bei ya $8,999 kwajili ya kununua Predator 21 X, Nitro 5 itaanza kuuzwa kwa $800 —inavutia, ama ?

Kwa upande wa utofauti wa mambo, unapata vibrant 15.6-inch FHD (1920 x 1080) IPS display, wakati Dolby Audio Premium na teknolojia ya Acer TrueHarmony  zinakupa uwezo wa ajabu wa sauti”. Tukiangalia CPU na GPU ni ngumu kufanya uchaguzi kwasababu “component permutations” nyingi tayari zinapatikana – kuna uchaguzi wa 7 Generation Intel Core i7 au i5 processors, au AMD 7th Generation AMD A-series FX, A12 or A10 APUs. Kisha kuna chaguzi za graphics hadi Nvidia GeForce GTX 1050 Ti au AMD Radeon RX550 graphics.

Laptop hii inakupa hadi 32GB ya DDR4 2400MHz memory. Baadhi ya mifano ni pamoja na PCIe SSDs (hadi 512GB) na hadi 2TB ya kuhifadhi kwenye HDD. Ports ni pamoja na Gigabit Ethernet, USB 3.1 Aina ya C, USB 3.0, USB 3.1 Type-C, USB 3.0, jozi ya USB 2.0 ports, na HDMI output. Kwajili ya kuunganisha wireless, laptop inaruhusu 802.11ac Wi-Fi na 2 x 2 MIMO antenna.

Makadilio ya bei ya laptop hii kwa fedha za kitanzania ni kama shilingi 1789600.

Kwa hari hii, nadhani OEMs wanatakiwa  kuacha kusafirisha Laptop zenye USB 2.0 mwaka 2017, aaaahn!

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

This article has 2 comments

  1. Amani Reply

    Kweli naona sasa Acer wanakimbizana na Dell(Alienware). Kwa kuleta mashine yenye uimara wa kucheza game kubwa kwenye soko la laptop, itawezesha watu wengi waweze kumiliki laptop hii na kufanya soko la “gaming” kompyuta kushuka bei

    • Benix Matrix Reply

      Kweli mkuu hapa lazima na Kampuni zingine zijitazame na kuangalia ubora na thamani ya vifaa vyao kwajili ya “gaming” soko la vifaa hivi naamini tararibu litashuka

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako