Home Nyingine Mbowe jisalimishe Polisi, Masogange, Chid Mapenzi, Wallis Nasher tumewakuta na madawa

Mbowe jisalimishe Polisi, Masogange, Chid Mapenzi, Wallis Nasher tumewakuta na madawa

0
1

Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm limemtaka m/kiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema kujisalimisha Polisi mara moja kwa ajili ya mahojiano yanahusuhu vita dhidi ya dawa za kulevya baada juhudi za kumsaka katika makazi yake kushindikana huku simu yake ya mkononi ikiwa imezimwa.

Akiongea kupitia East Africa Radio habari Kamanda Sirro amemtaka Mbunge na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe ambaye alitajwa kwenye majina 65 ya watu wanaojihusisha na Mihadarati kuripoti yeye mwenyewe Polisi kabla hatua za kijeshi hazijachukuliwa.

Kamanda Siro amesema Mbowe amejificha na anajua kuwa wanamtafuta wamtaka Jumatatu kuripoti Polisi.

Aidha jeshi hilo limesema watuhumiwa watatu Agnes Masogange,Rashid Iddi au Chid Mapenzi na Wallis Latif Nasher ambae ni muuza magari katika eneo la mikocheni watapandishwa kizimbani jumatatu kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya lakini pia walibainika wanatumia dawa hizo baada ya kupelekwa kwa mkemia mkuu.

Comment(1)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *