Nyingine

Je una bashiri “kubeti” ili kujikwamua na matatizo ya kimaisha ?

on


Kwa Mtanzania wa sasa ukisema neno “kubeti” anakuelewa moja kwa moja unachomaanisha, labda kwakuwa yeye mwenyewe ameshacheza au watu anaowajua, pengine hata kuwaona tu wengine.

Hii ni michezo ya bahati nasibu ambapo kampuni mbalimbali duniani huweka viwango fulani kwa mashabiki wa michezo hiyo kutabiri mwenendo wa mchezo husika utakavyokuwa au utakavyoisha.

Hapa Tanzania mchezo maarufu zaidi ni soka. Hivyo mashabiki wa mchezo huo hutabiri mambo kadhaa katika mchezo husika ikiwemo wafungaji wa magoli, idadi ya magoli kwenye mechi husika, magoli yatafungwa kipindi kipi cha mchezo, mechi ikiisha matokeo yatakuwaje, n.k.

SOMA NA HII:  Namna ya Kubeti na Kushinda Mkeka wa Pesa Nyingi

Matokeo yakiwa chanya, mashabiki hujinyakulia fedha kwa viwango tofauti kulingana na pointi ya timu alizochagua.

Swali ni, Je wewe una bashiri ili kujikwamua na matatizo ya kimaisha (kuboreka, kukosa furaha na maisha ya nyumbani n.k) ama kufurahisha nafsi tu ?

Toa maoni yako hapa chini.

Tuambie kwa nini wewe unapenda kubeti ?

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.