Simu

Google imenunua kitengo cha HTC cha kuunda smartphones

Google imesaini makubaliano na HTC ambayo yataleta talanta na ubunifu wa HTC kwenye kampuni hiyo kubwa ya kutafuta vitu mtandaoni.

Google imenunua HTC-mediahuru

HTC itapokea dola bilioni 1.1 kutoka Google kama malipo ya kuuza kitengo chake cha kuunda smartphones. Google pia itapokea leseni isiyo ya kipekee kwajili ya “HTC intellectual property”.

Google wanataka kupanua biashara yake ya simu. Wafanyakazi 2000 wa kampuni ya Taiwan HTC watajiunga na Google nchini Marekani.

Kundi la wafanyakazi kutoka HTC ambalo litajiunga na Google limefanya kazi na kampuni hiyo kwenye kuunda smartphone yake ya pixel.

“Kwa njia nyingi, mkataba huu ni agano la historia ya miaka kumi ya kufanya kazi kama timu kati ya HTC na Google,” alisema Google.

Makampuni hayo pia yalishirikiana kwenye kutengeneza Nexus One mwaka 2010, tablet ya Nexus 9 mwaka 2014, smartphone ya kwanza ya Pixel mwaka 2016, na smartphone ya kwanza ya Android.

“Tumezingatia kujenga uwezo wetu wa msingi, wakati wa kujenga portfolio ya bidhaa ambazo huwapa watu uzoefu wa kipekee.”

Malipo na makabidhiano, ambayo ni pamoja na vibali vya udhibiti,yanatarajiwa kukamilika mapema mwaka wa 2018.

SOMA NA HII:  Unakubali? Windows Kuzipita Android Tablets Ifikapo Mwishoni mwa 2017.
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Toa Maoni Hapa:

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako