Habari za Teknolojia

AfriCar Group inatafsiri tovuti zake katika lugha 10 ili kuongeza watumiaji

Africar Group, jukwaa la magari barani Afrika linalofanya kazi katika nchi 22 ndani ya bara hili sasa linapatikana katika lugha 10 za nchi mbalimbali ili kuhamasisha upatikanaji na matumizi kwa watu wa ndani na kupambana na kampuni ya  Cheki inayokua kwa kasi barani Afrika.

AfriCar Group inatafsiri tovuti zake katika lugha 10 ili kuongeza watumiaji-MEDIAHURUKwa ufanyaji kazi katika nchi 22 kwa njia ya tovuti za matangazo ya gari, kampuni hiyo inasema imewekeza  kwa watu wa ndani, na majukwaa yote yaliyokuwa yanapatikana katika lugha za Kiingereza na Kifaransa sasa yametafsiriwa kwa lugha za ndani ikiwa ni pamoja na lugha ya Kiamhari (Amharic), Kisomali, Kihausa, Kiyoruba, Kiswahili ,  Malagasy na hivi karibuni Wolof, Zulu, Sotho na Swazi ili watumiaji waweze kupata urahisi zaidi.

“Kutafsiri majukwaa yetu tofauti ina maana kubwa kwetu sisi tunapozingatia watu wa ndani. Tunataka waweze kufikia kwa urahisi tovuti zetu za matangazo ya gari ili waweze kufaidika na huduma hii ya bure. Kwa maana hiyo, tunafikiri kuwa ni muhimu kuyaboresha majukwaa yetu ya ndani na inafaa kwa watumiaji wetu. Sasa tunafikia mamilioni ya watumiaji wenye na sisi ni pekee kati ya washindani wetu kufanya jitihada hiyo na kuwapa huduma hii. “Anasema Axel Peyriere, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Africar Group.

Ina makao makuu huko Sydney, Australia, Africar Group inawezeshwa na wawekezaji wa kimataifa ikiendeshwa na timu ya watu 100+ wenye waendeshaji na mawakala katika kila nchi pamoja na wafanyakazi wa kudumu katika nchi nyingi.

SOMA NA HII:  Watumiaji Wa Simu Za Mkononi Afrika Kufikia Nusu Bilioni mwaka 2020

Tovuti za Africar Group ni pamoja na cargebeya.com nchini Ethiopia, carisoko.com nchini Rwanda, carisowo.com nchini Benin, carsugu.com nchini Burkina Faso, Carkibanda.com nchini Uganda, caryanga.com nchini Malawi, carsuq.com nchini Chad, mobili.com-Mali, caryandi.com nchini Zambia, cartsenga.com nchini Swaziland, caryange.com nchini Namibia, gaadhi.com nchini Somalia, voitures.ci nchini Ivory Coast, carasigbe.com huko Togo, carguinee.com nchini Guinea, carkugura.com katika Burundi, carmusika.com nchini Zimbabwe, carsotho.com nchini Lesotho, fiarakodia.com huko Madagascar, gaaraas.com nchini Senegal, motorokara.com nchini Botswana na voitures.ga huko Gabon.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

JIUNGE NA MAZUNGUMZO, TOA MAONI YAKO HAPA

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Lako