Watayarishaji wa video nyumbani kukimbilia kivuli cha bendera hakutosaidia.


Kumekuwa na lawama dhidi ya wasanii wa Bongo Fleva kwamba siyo wazalendo, hawapendi wala kuthamini vya nyumbani, ni watumwa wa kifikra wenye mitazamo hasi inayowaongoza kuamini kwamba ili wafanikiwe kisanaa lazima video za nyimbo zao wakazifanye nje ya nchi tena kwa kuwatumia waongozaji wa huko na kuwaacha Watanzania.

Ukiwauliza wasanii  “Kwa nini mnapenda kufanyia video za nyimbo zenu nje ya nchi na watayarishaji wasio Watanzania?’ utakutana na majibu mengi. Kila mmoja akijitetea kwa mtindo wake.

Wapo wanaosema eti watayarishaji wa nje wana vifaa bora na vya kisasa zaidi ukulinganisha na wazawa, wengine wanadai kuwa wanakwenda huko ili kutafuta chaneli za kujitangaza na kufahamika zaidi kwa madai kwamba watayarishaji hao wana mtandao mkubwa na imara wa wadau wa muziki Duniani.

Baadhi ya wasanii wanawashutumu watayarishaji wa Kitanzania kwamba wameishiwa ubunifu na hawana nidhamu ya kazi hasa kwenye suala zima la muda. Siyo hekima kupinga utetezi wanaotumia wasanii katika hili, lakini siyo sawa kukubali hata visivyostahili kukubalika.

Ukweli ni kwamba hilo sio jambo la kulaumu kwakuwa msanii ana haki ya kuamua wapi, nani na lini ashoot video yake. Mara nyingi uamuzi wa kutumia muongozaji wa nje hutokana na msanii kutaka kitu kikubwa zaidi ya anachoweza kupata nyumbani na nia ya wasanii wengi wa Tanzania kutaka kufanikiwa kimataifa pia.

Ongezeko la wasanii kuwatumia waongozaji wa nje ni ishara kuwa waongozaji wa ndani hawana ujuzi wa kutosha au ubunifu wa kufanya video nzuri. Tatizo ni nini? Producer Lucci amewahi kutaja sababu tatu kubwa: Vifaa, Ujuzi na Connections za waongozaji.

Hata hivyo kwa upande wa madirector wapo wanaopinga swala hili, Director mmoja amewahi kusema kuwa vifaa na ujuzi sio tatizo na kama wasanii wakiwalipa fedha ya uhakika, waongozaji wa Tanzania wanao uwezo wa kufanya video zenye ubora sawa na director wa nje. Je hilo ni kweli?

Video na film production kama sekta nyingine imefika sehemu ambapo uweledi ndio kinachohitajika, wasanii wataendelea kufanya lolote wawezalo kukuza Brand zao iwe kwa collabo za nje ama video etc. Directors nao wagundue ushindani umeingia na si kutegemea mavuno wakati haujapanda ni kujidanganya.

Wasanii wanaweza kuwa sahihi, siku hizi hamna ubunifu tena Bongo? madirector hawajitumi kwa bidii za kutosha kusonga mbele, Kazi zimekua hazina mvuto…. ubunifu ni kitu muhimu lakini haupo kwa sasa.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA