Roma na wenzake wako wapi ? Mastaa waguswa na tukio hilo


Stori ya Rapper Roma Mkatoliki na wenzake kukamatwa na watu wasiojulikana kwenye studio za Tongwe Records Dar es Salaam inaendelea kuchukua headlines mitandaoni.

Juhudi za mke wa Roma, Nancy zimegonga mwamba. Katika mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari, Nancy amesema amezunguka katika vituo vingi vikubwa vya polisi kuulizia taarifa za mumewe jibu analokutana nalo ni ‘hatuna taarifa zozote, tutashughulikia’.

“Serikali, waandishi wa habari, Watanzania, yeyote aliyeona, aliyesikia, anayeweza kutusaidia Roma yuko wapi naombeni msaada wenu,” amesema Nancy.

“Nahitaji kufahamu yuko wapi, yuko katika hali gani,” .

Roma na wenzake wako wapi ? Ni swali ambalo kila mtu anajiuliza kwa sasa? Wasanii wengi wameingiwa na hofu kubwa. Haya ni baadhi ya maoni yao:

#Repost @mubenga with @repostapp ・・・ #FreeRoma

A post shared by Kajala Masanja (@new_kajala) on

nADHANI SASA NI MUDA WA KUFOKAFOKA.

A post shared by #wANANDOTO? (@kalajeremiah) on

KAULI YA MMILIKI WA TONGWE RECORDS @j_murder_tongwe VIVA ROMA VIVA

A post shared by Professor Jay (@professorjaytz) on

Tusifikie huku jamani.warudisheni vijana wa watu.mnaogopesha wengi .hii sio Tanzania tunayoitaka wallah.

A post shared by malkia wa mipasho duniani (@officialkhadijakopa) on

Vanessa Mdee

SOMA NA HII:  Boss wa Facebook Kujibu tuhuma za Kutumia Data Kwenye Bunge la Uingereza

Wherever you are, God is Bigger than, Stronger than, Realer than all the other forces that be. Stay UP brother @roma2030 #VivaRoma #FreeRoma #FreeMoni roho inauma na nimetoka kumsikiliza mkeo redioni hajui hata ulipo sasa ndiyo nini ?????is this where we are at now? Ma studio yanavamiwa, watu wanakamatwa kama wanyama pori. Aaaarrrrgh

Ray C

Nimeanza kuingiwa na woga,nafikiria mambo mengi Roma alipo Sasa,anafanywa nini na tatizo ni nini mpaka imekuwa hivi na masaa yanaenda hakuna jibu lililo kamili!!hisia mchanganyiko na zote sio nzuri….Nini kinaendelea?Tatizo ni nini??Sababu ni nini?Bado najiuliza sipati jibu………

SOMA NA HII:  Boss wa Facebook Kujibu tuhuma za Kutumia Data Kwenye Bunge la Uingereza

Fid Q

Nimeipokea hii HABARI kwa mstuko mkubwa.. sio tu kwasababu TONGWE ni moja kati ya wadhamini wetu wa #OpenMicThursday pia ni moja kati ya studio ambazo zimekua msaada mkubwa sana ktk kunyanyua vipaji na C E O @j_murder_tongwe amekua mstari mbele sana ktk kufanikisha hilo.. kinachonistua na kuninyima raha zaidi ni hili la hawa ndugu zetu akina @roma2030 @moni_centrozone Producer Belo na mlinzi kuwa hawajulikani waliko hadi hivi sasa.. ninaiomba MAMLAKA HUSIKA ya USALAMA itusaidie ili waweze kupatikana mapema na kuifutilia mbali ile hofu iliyotanda mioyoni mwa ndugu, jamaa na marafiki… mwisho namuomba MUWEZA WA VYOTE azifanyie wepesi familia za ndugu zetu waliopotelea kusikojulikana in sha Allah

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA